10 Wakalia kwa sauti kuu wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, utakawia mpaka lini kuwa hukumu na kulipiza kisasi juu ya watu wote waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” 11 Kisha kila mmoja wao akapewa kanzu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kidogo zaidi mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao wanaopaswa kuuawa kama wao walivyouawa, ita kapotimia.

12 Nilitazama Mwana-Kondoo alipokuwa akifungua muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi. Mwezi wote ukawa mwekundu kama damu.

Read full chapter