Font Size
Ufunua wa Yohana 6:11-13
Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 6:11-13
Neno: Bibilia Takatifu
11 Kisha kila mmoja wao akapewa kanzu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kidogo zaidi mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao wanaopaswa kuuawa kama wao walivyouawa, ita kapotimia.
12 Nilitazama Mwana-Kondoo alipokuwa akifungua muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi. Mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka ardhini kama vile mat unda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapoti kiswa na upepo mkali.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica