Akatoka farasi mwingine mwekundu sana na aliyempanda alipewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye alipewa upanga mkubwa.

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tatu, nilimsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikaona farasi mweusi, na aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. Nikasikia kitu kama sauti kati ya hao viumbe wanne hai, ikisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa mshahara wa siku moja! na vibaba vitatu vya shayiri kwa mshahara wa siku moja! Lakini usi haribu mafuta wala divai!”

Read full chapter