Font Size
Ufunua wa Yohana 6:6-8
Neno: Bibilia Takatifu
Ufunua wa Yohana 6:6-8
Neno: Bibilia Takatifu
6 Nikasikia kitu kama sauti kati ya hao viumbe wanne hai, ikisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa mshahara wa siku moja! na vibaba vitatu vya shayiri kwa mshahara wa siku moja! Lakini usi haribu mafuta wala divai!”
7 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa nne, nilisikia sauti ya yule kiumbe hai wa nne ikisema, “Njoo!” 8 Nikaangalia na mbele yangu nikamwona farasi mwenye rangi ya kijivu. Aliyempanda huyo farasi aliitwa mauti, naye alikuwa akifuatana na kuzimu. Nao wal ipewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica