Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa nne, nilisikia sauti ya yule kiumbe hai wa nne ikisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikamwona farasi mwenye rangi ya kijivu. Aliyempanda huyo farasi aliitwa mauti, naye alikuwa akifuatana na kuzimu. Nao wal ipewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tano, niliona chini ya madhabahu, roho za watu waliouawa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ushuhuda wao.

Read full chapter