kabila la Simioni 12,000, kabila la Lawi 12,000, kabila la Isakari 12,000, kabila la Zabuloni 12,000, kabila la Yusufu 12,000, kabila la Benyamini 12,000.

Umati Wa Watu Waliokombolewa

Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu ambao hakuna mtu awezaye kuwahesabu: watu wa kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.

Read full chapter