Umati Wa Watu Waliokombolewa

Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu ambao hakuna mtu awezaye kuwahesabu: watu wa kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10 Nao walikuwa wakisema kwa sauti kuu, “Ukombozi hutoka kwa Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo!” 11 Na wale malaika wote wakasi mama kuzunguka kile kiti cha enzi na wale wazee na wale viumbe hai wanne, wakaanguka chini mbele ya kile kiti cha enzi wakamwab udu Mungu,

Read full chapter