11 Nyota hiyo inaitwa “Uchungu”. Theluthi moja ya maji yakawa machungu, na watu wengi walikufa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.

12 Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta, na theluthi moja ya jua, theluthi moja ya mwezi na theluthi moja ya nyota, zika pigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga wao ukawa giza. Theluthi moja ya mchana ilikuwa haina mwanga na pia theluthi moja ya usiku.

13 Halafu tena nikatazama, nikasikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, “Ole wao! Ole wao! Ole wao watu waishio duniani wakati itakaposikika milio ya tarumbeta ambazo karibuni zitapigwa na malaika watatu waliobakia.”

Read full chapter