Kisha nikawaona wale mal aika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, alikuja akasimama mbele ya madhabahu. Akapewa ubani mwingi auchanganye pamoja na sala za watu wote wa Mungu, kwenye madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kile kiti cha enzi. Ule moshi wa ubani ukapanda juu mbele za Mungu, pamoja na maombi ya watu wa Mungu , kutoka mkononi mwa huyo malaika.

Read full chapter