Halafu yule malaika akachukua kile chetezo akakijaza moto kutoka kwenye ile madhabahu akautupa juu ya nchi. Pakatokea radi, ngurumo, umeme na tetemeko la nchi.

Tarumbeta Za Kwanza Nne

Kisha wale malaika saba waliokuwa na tarumbeta saba waka jiandaa kuzipiga. Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, ikanyesha kwa nguvu juu ya nchi; na theluthi moja ya nchi ikateketea, na theluthi moja ya miti ikateketea na majani yote mabichi yakateke tea.

Read full chapter