Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, ikanyesha kwa nguvu juu ya nchi; na theluthi moja ya nchi ikateketea, na theluthi moja ya miti ikateketea na majani yote mabichi yakateke tea.

Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikageuka kuwa damu, theluthi moja ya viumbe hai waishio bahar ini wakafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.

Read full chapter