Tarumbeta Ya Tano

Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake, nikaona nyota iliyokuwa imeanguka kutoka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ili pewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Alipolifungua hilo shimo, moshi ulitoka ndani yake kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vilitiwa giza kwa ajili ya ule moshi uliotoka katika shimo hilo. Kisha, katika ule moshi wakatoka nzige wakatua ardhini. Nao wakapewa nguvu kama nguvu ya nge wa duniani.

Read full chapter