17 Na hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: wapanda farasi walivaa ngao vifuani zenye rangi ya moto na samawati na kiberiti. Na vichwa vya farasi hao vilikuwa kama vichwa vya simba; na moto, moshi na kiberiti vili kuwa vinatoka vinywani mwao. 18 Theluthi moja ya wanadamu waliu awa kwa maafa hayo matatu, yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliy otoka vinywani mwa hao farasi. 19 Nguvu ya hao farasi ilikuwa vinywani mwao na mikiani mwao; kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka wenye vichwa ambavyo vilitumika kuwadhuru watu.

Read full chapter