19 Nguvu ya hao farasi ilikuwa vinywani mwao na mikiani mwao; kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka wenye vichwa ambavyo vilitumika kuwadhuru watu.

20 Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika maafa hayo, bado walikataa kutubu na kuacha kuabudu vitu walivyotengeneza kwa mikono yao wenyewe. Waliendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, sanamu zisizoweza kuona, kusikia wala kutembea. 21 Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati na wizi.

Read full chapter