Kisha, katika ule moshi wakatoka nzige wakatua ardhini. Nao wakapewa nguvu kama nguvu ya nge wa duniani. Waliambiwa wasidhuru nyasi za nchi, wala majani, wala mmea au mti wo wote. Bali wawadhuru wale watu wasiokuwa na muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. Waliruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano lakini wasiwaue. Na uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama uchungu wa mtu anapoumwa na nge.

Read full chapter