Wale nzige walionekana kama farasi waliotayarishwa kwa vita; vichwani mwao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu; na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. Manyoya yao yalifanana kama nywele za wanawake; na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Walikuwa na magamba yaliyofanana na ngao za chuma; na kelele za mabawa yao zilikuwa kama kelele za magari ya farasi yenye farasi wanaokimbia kwenda vitani.

Read full chapter