Walikuwa na magamba yaliyofanana na ngao za chuma; na kelele za mabawa yao zilikuwa kama kelele za magari ya farasi yenye farasi wanaokimbia kwenda vitani. 10 Walikuwa na mikia ya kuuma kama nge; nguvu yao ya kutesa watu kwa muda wa miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. 11 Walikuwa na mfalme wa kuwatawala, naye ni malaika wa shimo la kuzimu ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Aba doni na kwa Kigiriki ni Apolioni.

Read full chapter