Font Size
Ufunuo 18:16-18
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 18:16-18
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
16 Watasema:
“Inatisha! Inatisha kwa mji mkuu!
Alivalishwa kitani safi;
alivaa zambarau na nguo nyekundu.
Alikuwa anang'aa kwa sababu ya dhahabu, vito na lulu!
17 Utajiri wote huu umeteketezwa kwa saa moja!”
Kila nahodha, wote ambao husafiri katika meli, mabaharia na wote ambao hupata pesa kutokana na bahari walisimama mbali na Babeli. 18 Waliuona moshi wa kuungua kwake. Walilia kwa sauti, “Hakukuwa na mji kama mji huu mkuu!”
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International