Font Size
Ufunuo 6:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 6:10-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
10 Roho hizi zilipiga kelele kwa sauti kuu zikisema, “Mtakatifu na Bwana wa kweli, ni lini utakapowahukumu watu wa dunia na kuwaadhibu kwa kutuua sisi?” 11 Kisha kila mmoja wao alipewa kanzu ndefu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kwa muda mfupi kwani bado walikuwepo ndugu zao katika utumishi wa Kristo ambao ni lazima wauawe kama wao. Roho hizi ziliambiwa zisubiri mpaka mauaji yote yatakapokwisha.
12 Kisha nilitazama wakati Mwanakondoo anaufungua muhuri wa sita. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi na jua likawa jeusi kama gunia jeusi[a] na mwezi wote ukawa mwekundu kama damu.
Read full chapterFootnotes
- 6:12 gunia jeusi Gunia lililofumwa kwa nyuzi za manyoya maeusi.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International