Font Size
Ufunuo 6:4-6
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 6:4-6
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
4 Nilipotazama nilimwona farasi mwekundu akitokea. Aliyekuwa anamwendesha farasi huyu alipewa mamlaka ya kuondoa amani duniani ili watu wauane. Alipewa upanga mkubwa.
5 Mwanakondoo alipoufungua muhuri wa tatu. Nilisikia kiumbe mwenye uhai wa tatu akisema, “Njoo!” Nilipotazama nilimwona farasi mweusi mbele yangu. Aliyekuwa anamwendesha farasi huyu alikuwa na mizani mkononi mwake. 6 Kisha nilisikia kitu kilichosikika kama sauti ikitokea pale walipokuwa viumbe wenye uhai wanne. Kikisema, “Kilo moja[a] ya ngano au kilo tatu ya shayiri itagharimu mshahara wote wa siku moja. Lakini usiharibu upatikanaji wa mafuta ya mzeituni na divai!”
Read full chapterFootnotes
- 6:6 Kilo “Kibaba au posho,” kiasi cha gawio la nafaka kwa ajili ya askari. Ni kama kilo moja.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International