Add parallel Print Page Options

13 Kisha mmoja wa wazee akaniuliza, “Watu hawa waliovaa kanzu nyeupe ni akina nani? Wametoka wapi?”

14 Nikajibu, “Wewe unajua ni akina nani, bwana.”

Mzee akasema, “Hawa ni wale waliokuja kutokana na mateso makuu. Wamefua kanzu zao[a] kwa kutumia damu ya Mwanakondoo, wako safi na ni weupe. 15 Hivyo sasa watu hawa wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Wanamwabudu Mungu mchana na usiku hekaluni mwake. Naye aketiye kwenye kiti cha enzi atawalinda.

Read full chapter

Footnotes

  1. 7:14 Wamefua kanzu zao Inamaanisha kwamba walimwamini Yesu na wamesafishwa dhambi zao kwa sadaka ya yake ya damu. Tazama Ufu 5:9; Ebr 9:14; 10:14-22; Mat 22:16; 1 Yoh 1:7.