Add parallel Print Page Options

Mlio wa Tarumbeta ya Sita

13 Malaika wa sita alipopuliza tarumbeta yake, nilisikia sauti ikitoka katika pembe[a] zilizo katika pembe[b] nne za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu. 14 Ikamwambia malaika wa sita aliyekuwa na tarumbeta, “Wafungue huru malaika wanne waliofungwa pembezoni mwa mto mkuu Frati.” 15 Malaika hawa wanne walikuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hii, siku hii, mwezi na mwaka huu. Malaika waliachwa huru ili waue theluthi moja ya watu duniani.

Read full chapter

Footnotes

  1. 9:13 pembe Kama za mnyama.
  2. 9:13 pembe Au “kona”.