Font Size
Ufunuo 9:19-21
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 9:19-21
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
19 Nguvu ya farasi ilikuwa kwenye midomo na mikia yao. Mikia yao ilikuwa kama nyoka walio na vichwa vya kuwauma na kuwadhuru watu.
20 Watu wengine duniani hawakufa kwa mapigo haya. Lakini watu hawa bado hawakubadili mioyo yao na kuacha kuabudu vitu walivyovitengeneza kwa mikono yao wenyewe. Hawakuacha kuabudu mapepo na sanamu zilizotengenezwa kwa dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, au kusikia au kutembea. 21 Hawakubadili mioyo yao na kuacha kuua watu wengine au kuacha uchawi, dhambi ya uzinzi na wizi.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International