Yesu Kristo ni yule yule, jana, leo na hata milele. Msipotoshwe na mafundisho ya kigeni ya namna mbalimbali. Ni vema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, na wala si kwa kutii mash arti kuhusu vyakula, ambavyo havina faida kwa wanaovila. 10 Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaohudumu katika hema ya kuabudia hawana haki ya kula vitu vilivyowekwa juu yake.

Read full chapter