10 kwa maana Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado hajazaliwa. Mbegu yake ilikuwa bado iko mwilini mwa Abrahamu babu yake.

Yesu Na Melkizedeki

11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria.

Read full chapter