27 Yeye hahitaji kutoa dhabihu kila siku kwa ajili ya dhambi zake kwanza kisha dhambi za watu, kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu mara moja kwa wakati wote, alipojitoa mwenyewe. 28 Kwa maana sheria ya Mose huchagua watu wenye udhaifu kuwa makuhani wakuu. Lakini neno la Mungu la kile kiapo ambalo lilikuja baada ya sheria, lil imteua Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.

Read full chapter