Angalieni jinsi alivyo mkuu! Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. Hata wana wa Lawi ambao ni makuhani, wameamriwa na sheria ya Mose kuwatoza Waisraeli ndugu zao, ambao ni wazao wa Abrahamu, sehemu ya kumi ya mapato yao. Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu.

Read full chapter