Add parallel Print Page Options

Unaweza kuona kuwa Melkizedeki alikuwa mkuu sana. Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa yeye sehemu ya kumi ya kila alichoshinda kule vitani. Sasa sheria inasema kwamba wale wa ukoo wa Lawi waliokuja kuwa makuhani wanastahili kupata sehemu ya kumi kutoka kwa watu wao, hata kama wao na watu wao ni wa familia ya Ibrahimu. Melkizedeki wala hakutoka katika kabila la Lawi, lakini Ibrahimu akampa sehemu ya kumi ya alivyokuwa navyo. Na Melkizedeki akambariki Ibrahimu yule aliyekuwa na ahadi za Mungu.

Read full chapter