Hata wana wa Lawi ambao ni makuhani, wameamriwa na sheria ya Mose kuwatoza Waisraeli ndugu zao, ambao ni wazao wa Abrahamu, sehemu ya kumi ya mapato yao. Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu. Wala hakuna ubishi kuwa mtu mdogo hubarikiwa na mtu aliye mkuu kuliko yeye.

Read full chapter