Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu. Wala hakuna ubishi kuwa mtu mdogo hubarikiwa na mtu aliye mkuu kuliko yeye. Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi.

Read full chapter