Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi. Mtu anaweza kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, 10 kwa maana Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado hajazaliwa. Mbegu yake ilikuwa bado iko mwilini mwa Abrahamu babu yake.

Read full chapter