Add parallel Print Page Options

Sasa wale wa kutoka ukoo wa Lawi ndiyo wanaopata sehemu ya kumi kutoka kwa watu. Lakini tunaweza kusema kuwa Ibrahimu alipompa Melkizedeki sehemu ya kumi, kisha Lawi naye akatoa. 10 Lawi alikuwa bado hajazaliwa, lakini alikuwepo katika baba yake Ibrahimu wakati Melkizedeki alipokutana naye.

11 Watu walipewa sheria chini ya mfumo wa makuhani waliotoka katika ukoo wa Lawi. Lakini hayupo awezaye kufanywa mkamilifu kiroho kwa njia ya mfumo wa makuhani. Hivyo lilikuwepo hitaji la kuhani mwingine kuja. Namaanisha kama Melkizedeki, siyo Haruni.

Read full chapter