Kila kuhani huteuliwa ili atoe sadaka na dhabihu, kwa hiyo ilikuwa muhimu kwamba huyu kuhani naye awe na kitu cha kutoa. Kama angalikuwa duniani asingalikuwa kuhani kwa sababu wapo makuhani wanaotoa sadaka kwa mujibu wa sheria ya Mose. Wanahu dumu katika patakatifu iliyo mfano na kivuli cha ile iliyoko mbinguni. Ndio maana Mose alipokaribia kujenga ile hema takatifu aliamriwa na Mungu, akisema, “Hakikisha kuwa unafanya kila kitu kulingana na mfano ulioonyeshwa mlimani.”

Read full chapter