Add parallel Print Page Options

Kila kuhani mkuu anayo kazi ya kutoa sadaka na sadaka kwa Mungu. Hivyo kuhani wetu mkuu pia anahitajika kutoa kitu kwa Mungu. Kama kuhani wetu mkuu angekuwa anaishi duniani, asingekuwa kuhani. Nasema hivi kwa sababu tayari hapa wapo makuhani ambao wanafuata sheria kwa kutoa sadaka kwa Mungu. Kazi ambayo makuhani hawa wanafanya hakika ni nakala tu na kivuli cha yaliyoko mbinguni. Ndiyo sababu Mungu alimwonya Musa alipokuwa amejiandaa kujenga Hema Takatifu: “Uwe na uhakika kufanya kila kitu sawasawa na kielelezo nilichokuonesha kule mlimani.”(A)

Read full chapter