Kwa hiyo mtakaposoma barua hii mtaweza kutambua ufahamu niliopewa kuhusu siri ya Kris to. Siri hii haikufahamika kwa watu wa vizazi vilivyopita kama ilivyodhihirishwa sasa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa mataifa ni warithi pamoja na Waisraeli; na wote pamoja ni viungo vya mwili mmoja, na ni washiriki kwa pamoja wa ile ahadi aliyotoa Mungu katika Kristo Yesu.

Read full chapter