Niliteuliwa kuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa uwezo wake uliokuwa ukifanya kazi ndani yangu. Ingawa mimi ni mdogo kuliko hata aliye mdogo kabisa kati ya watu wote wa Mungu, nilipewa neema hii, niwahubirie watu wa mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo. Na nieleze wazi wazi ili watu wote waone jinsi siri hii itakavyotekelezwa. Siri hii ilikuwa imefichwa tangu awali kwa Mungu aliyeumba vitu vyote.

Read full chapter