10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Read full chapter