18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. 19 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo.

Read full chapter