20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo. 21 Ndugu mpendwa Tikiko, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawaelezeni kila kitu ili mjue habari zangu na mfahamu ninachofanya. 22 Ninamtuma kwenu kwa kusudi hili, mpate habari zetu naye awafariji.

Read full chapter