Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu.

Read full chapter