Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Read full chapter