Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu.

Read full chapter