12 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba haya mambo yaliyonipata yamesaidia sana kueneza Injili ya Kristo. 13 Watu wote hapa pamoja na maaskari wa ikulu wanajua wazi kuwa mimi niko kifungoni kwa sababu ya kumtumikia Kristo. 14 Kwa sababu ya kifungo changu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu pasipo hofu.

Read full chapter