Add parallel Print Page Options

13 Walinzi wote wa Kirumi na wengine wote hapa wanafahamu kuwa nimefungwa kwa sababu ninamtumikia Kristo. 14 Kufungwa kwangu gerezani kumesababisha waamini walio wengi hapa kuweka tumaini lao kwa Bwana, na kuhubiri ujumbe wa Mungu kwa ujasiri mwingi pasipo woga.

15 Baadhi ya watu wanahubiri ujumbe wa Kristo kwa sababu wananionea wivu na wanataka watu wawafuate wao badala yangu. Wengine wanahubiri kwa sababu wanataka kusaidia.

Read full chapter