14 Kwa sababu ya kifungo changu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu pasipo hofu. 15 Ni kweli kwamba wapo ndugu wengine wanaom hubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. 16 Hawa wanahubiri kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba Mungu ameniweka hapa kifungoni ili niitetee Injili.

Read full chapter