Nina hakika kwamba, yeye aliyeianza kazi yake njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha siku ile ataka porudi Yesu Kristo.

Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu.

Read full chapter