Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu. Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara

Read full chapter