Add parallel Print Page Options

Habari Njema hii inahusu Mwana wa Mungu, ambaye kama mwanadamu, alizaliwa katika ukoo wa Mfalme Daudi. Na alipofufuliwa na Roho Matakatifu[a] kutoka kwa wafu, alipewa mamlaka kamili ya kutawala kama Mwana wa Mungu. Ni Yesu Kristo, Bwana wetu.

Kupitia kwa Yesu, Mungu amenionyesha wema wake. Na amenipa mamlaka ya kuwaendea watu wa mataifa yote na kuwaongoza kumwamini na kumtii yeye. Kazi yote hii ni kwa ajili yake.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:4 Roho Matakatifu Kwa maana ya kawaida, “Roho wa Utakatifu”.