19 Kwa hiyo basi, tufanye kila juhudi tutimize yale yaletayo amani na kujengana. 20 Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Vyakula vyote vinafaa, lakini ni kosa kula kitu ambacho kinamfanya mwenzako kujikwaa. 21 Ni afadhali usile nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lo lote litakalomfanyandugu yako aanguke.

Read full chapter