Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini. Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Read full chapter